MCHUNGAJI ANAISHI NA WAKE ZA WATU KAGERA

Mchungaji Japhes Josephat ambaye ni mmiliki wa kanisa la Kipentekoste la ‘Huruma Katika Kristo’ anadaiwa kuishi na wake wa waumini wake kwa kile anachodai kushukiwa na Roho Mtakatifu

Kufuatia hali hiyo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera imelazimika kuhamia kwa muda katika kanisa hilo la kipentekoste la ‘Huruma Katika Kristo’ kwa ajili ya kuchunguza jambo hilo.

Mbali na hilo mchungaji huyo anadaiwa pia kukatisha masomo ya baadhi ya wanafunzi katika kijiji cha Nyakintuntu ambao wamejiunga na kanisa lake hilo.

 

Facebook Comments