Maporomoko ya mawe yazua taharuki Tanga

Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Benedict Wakuyamba amewataka madereva kuacha tabia ya kuendesha magari yao kwa mazoea wakati huu wa mvua kwa sababu barabara nyingi zinaharibika.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamishna huyo amesema hali ya mvua imekuwa kubwa katika mkoa huo na kupelekea baadhi ya barabara kufunikwa na matope pamoja na miti mikubwa ambayo inapelekea kuleta ugumu wa usafiri.
“Hali ya mvua imeendelea kunyesha na kufukia barabara eneo la Mombo kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha ambapo matope na miti vimesombwa na kukwama barabarani hali iliyokwamisha magari makubwa kwa madogo kusafiri kupitia eneo hilo..Niwaombe abiria au wananchi kwa ujumla kama hawana ulazima wa kusafiri kwenda mikoa ya Kaskazini ni vizuri wakatulia kwa siku mbili tuone hali inakwendaje kwa ajili ya usalama wao”. Alisema Kamishna Msaidizi Benedict
Kwa uapnde mwingine Kamishna huyo amesema TANROADS na Jeshi la Polisi mkoani humo wanaendelea kusaidia kuondoa magogo na tope zilizosakama katika barabara ili kunusuru hali ya usafiri.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*