Serikali Yatoa Agizo la Kukamatwa Aliyemjeruhi Mtoto Kwa Kosa la Kutokoa Chakula

WIZARA: YASISITIZA KUKAMATWA KWA ALIYEMJERUHI MTOTO KWA KOSA LA KUDOKOA CHAKULA
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imelaani vikali kitendo cha mtoto wa miaka mitatu (jina limehifadhiwa), mkazi wa kata ya Rudete mkoani Geita, ambaye amejeruhiwa na mama wa kambo kwa kuchomwa moto mwilini akituhumiwa kuiba chakula alichobakiziwa baba yoke.

Wizara imesikitishwa na tukio hili rnaana linakinzana na kaulimbiu ya Madhirnisho ya Siku ya Kirnataifa ya Familia kota mwaka 2017, ambayo pamoja na mambo mengine, inasisitiza wazazi na walezi, kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wa kuimarisha malezi kwa ajili ya ustawi wa watoto katika familia na jamii kwa ujumla.

Katika kutekeleza utoaji no haki za Mtoto na ustawi wake, wadau note wanaotoa huduma kwa mtoto wanasisitizwa kusimamia upatikanaji no haki tote za msingi katika familia na jamii, ikiwemo haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushirikishwa na kutobaguliwa.

Wizara inawaomba wananchi kote nchini kutoa ushirikiano katika kuwafichua wanaotenda vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika, iii kuhakikisha wahusika wa vitendo vya ukatili wanachukuliwa hatua.

Napenda kutoa maelekezo kwa Maafisa Maendeleo, Ustawi wa Jamii wa kuhakikisha kuwa mtoto huyo anapatiwa huduma ya matibabu haraka iii kumrejesha katika afya njema.

Kwa vile, jukumu la ulinzi na usalama wa mtoto linatekelezwa kwa ushirikiano mkubwa wa Polisi, tunaamini kuwa suala hit linatafuatiliwa kuhakisha kuwa watuhumiwa no vitendo hivi vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya huyo mtoto mdogo wanapatikana.

Azma ya Wizara yen ye dhamana ya Watoto, ni kuhakikisha kuwa familia zinaendelea kuwa kitovu cha upatikanji wa haki, ustawi na maendeleo kwa maslahi ya watoto wetu.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*