Taadhali Kwa Umma Kuhusu Ajira Zitazotolewa na TAMISEMI

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BARUA ZA KUGUSHI ZA WATAALAMU WA AFYA KWENYE MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushirikiana na Wizara Mya ilitangaza ajira na kuwapangia vituo vya kazi Wataalam wapya wa Afya kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri , Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Hivi karibuni kumezuka tabia ya utapeli inayofanywa na mtu anayejiita N.M.Mhoji kama mtumishi anayefanya kazi Ofisi ya Rais TAMISEMI ambaye anatoa barua kwa jina lake na kuwapangia vituo vya kazi Wataalam hao. Kimsingi barua hizo si halisi (ni feki), na zinatungwa na watu wenye lengo la kuichafua Serikalini hususani Ofisi ya Rais TAMISEMI lakini pia wana lengo la kujipatia fedha kwa njia .Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEM() inapenda kuchukua fursa hii, kutoa taarifa hii kwa lengo la kujulisha Umma wa Watanzania ya kuwepo kwa uhalifu huu waweze kujiepusha nao.

Ofis ya Rais – TAMISEMI haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa wale wote watakaobaiMka kujihusisha na uhalifu wa aina hii. Ofisi ya Rais- TAMISEMI inawasisitizia Waajiri ambao ni Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za serikali zaMitaa kuwa wazingatie tangazo na orodha halisi ya waajiriwa ambayo inapatikana katika tovuti za Ofisi ya Rais TAMISEMI www.tamisemi.go.tz na Wizara ya Afya www.moh.go.tz na pia hakuna barua yoyote iliyotolewa kwa waajiriwa hao.

Facebook Comments