Nafasi 145 za kazi Ofisi za Takwimu elimu kunzia kidato cha Nne

TANGAZO LA KAZI – NAFASI 145 ZA WADADISI
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inapenda kuwatangazia nafasi za kazi ya muda ya udadisi au ukusanyaji wa takwimu kwa ajili ya miradi ifuatayo:
i. Utafiti wa Msingi wa Matumizi ya Ardhi kwa Mwaka 2017/18 katika wilaya za Kilombelo, Ulanga na Malinyi.

ii. Utafiti wa Awamu ya Pili wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania,

Waombaji wanatakiwa kuwa ni Watanzania wenye sifa zifuatazo;
i. Umri wa miaka 18 na kuendelea,

ii. Elimu ya kuanzia Kidato cha Nne,

iii. Elimu ya ngazi ya Shahada, Stashahada, Astashahada katika Takwimu rasmi au Cheti cha Ukusanyaji Takwimu rasmi, kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC),

iv. Uwezo wa kutumia Tablets na CAPI wakati wa kukusanya takwimu.
Aidha, Barua za maombi zilizoandikwa kwa mkono zikiambatishwa na nakala za vyeti husika zitumwe Ofisi ya Taifa ya Takwimu Makao Makuu kabla ya tarehe 31/05/2017 kwa kupitia anuani ifuatayo;
Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, 18 Barabara ya Kivukoni, S.L.P 796, 11992 DAR ES SALAAM.
NB: i. Tangazo hili linapatikana kupitia www.nbs.go.tz pamoja na www.eastc.ac.tz
ii. Wale watakaochaguliwa kwa ajili ya usaili ndio watakaoitwa. NBS haitahusika na gharama za kuja kwenye usaili huu.
MKURUGENZI MKUU OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU

17 Mei, 2017

BONYEZA HAPA KUTEMBELEA MTANDAO WAO

Facebook Comments