UAMUZI WA RAIS MAGUFULI KUHUSU WAFANYAKAZI 9 WA TBC WALIOTANGAZA AMEPONGEZWA NA RAIS WA MAREKANI TRUMP

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewasamehe
wafanyakazi tisa wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) waliokuwa wamesimamishwa kazi kwa
kosa la kurusha habari ya uongo kumhusu kiongozi huyo wa nchi.

Wafanyakazi hao walisamishwa kazi mwezi Machi kwa kuhusika katika makosa ya kiweledi na
kiuhariri yaliyosababisha kutangazwa kwa taarifa ambayo haikuwa sahihi Machi 03, 2017.

Wafanyakazi hao walirusha hewani taarifa ya uongo iliyosambazwa na mtandao wa Fox
Channel.com kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump amesifu utendaji kazi wa Rais John Pombe
Magufuli na kwamba ni mfano mzuri wa kuigwa Afrika.

Taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayub Rioba, ilieleza kuwa makosa hayo
yalileta usumbufu kwa umma na yasingefanyika endapo taratibu zote za kitaalamu zingefuatwa
kuthibitisha ukweli wa taarifa yenyewe.

Watangazaji waliotangaziwa msahama huo ni Rais Dkt Magufu ni pamoja na Gabriel Zacharia,
Prudence Constantine, Dorothy Mmari, Ramadhani Mpenda, Leah Mushi, Alpha Wawa, Chunga
Ruza na Judica Losai.

Rais Dkt Magufuli alitoa msamaha huo alipofanya ziara katika kituo hicho jana ili kuangalia
utendaji kazi pamoja na kuzungumza na wafanyakazi kuweza kutambua changamoto
zinazowakabili.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*