Chidi Benz: Sijawahi kupokea pesa nilizochangiwa

Chid Benz akiwa na Babu Tale, Kushoto ni cover ya ngoma yake mpya

Rapa mkongwe kutoka ‘La Familia’, Chidi Benz amekana kupokea pesa yoyote aliyochangiwa na wapenzi na mashabiki zake katika kipindi ambacho alikuwa akikabiliwa na matatizo.

Kauli hiyo imekuja kutokana na kuwepo kwa taarifa za baadhi ya watu kuendesha kampeni ya kumchangia nyota huyo ili apate matibabu baada ya kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

Chid amamesema katika kipindi kipindi chote ambacho hali yake ilikuwa mbaya, hakuwahi hata kusikia mchakato huo wa michango, huku akisisitiza kuwa uwezo alionao wa kufanya muziki pamoja na kazi za muziki alizokwishafanya vina thamani zaidi ya kiasi chochote cha pesa ambazo zitakuwa zimechagwa, hivyo hawezi kuzifuatilia pesa pesa hizo hata kama ni milioni 200.

Katika hatua nyingine Chidi amesema hajawahi kuwa na meneja katika maisha yake ya muziki, na kukanusha taarifa zinazodai kuwa Babu Tale amewahi kuwa meneja wake.

“Babu Tale ni mtu watu wa karibu, alikuwa akinipa ideas na tunazifanyia kazi, lakini hakuwahi kuwa meneja wangu, mimi sina meneja wala sijawahi kuwa na meneja” Amesisitiza Chidi

Hivi sasa Chidi amerudi upya kwenye game akitoka na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina muda, na yuko katika harakati za kukamilisha video ya ngoma hiyo.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*