Mmoja ‘achinjwa’ uchaguzi Mkuu TFF

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus Kuuli (Katikati) akiwa pamoja na wajumbe wengine wa kamati hiyo.

Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF imepitisha majina 73 ya wagombea katika nafasi mbalimbali huku ikikata jina moja na Abdallah Musa aliyekuwa akigombea ujumbe

Taarifa iliyotolewa na kamati hiyo ni kwamba mgombea huyo kutoka Kanda Na. 1 ya mikoa ya Kagera na Geita amekatwa kutokana na kutoambatanisha kivuli cha cheti cha kidato cha nne kwa mujibu wa kanuni ya 9 inayozungumzia sifa nane za kuwania uongozi TFF.

Wagombea wote waliobaki wametakiwa kufika kwenye usaili utakaofanyika kuanzia Juni 29, 2017 hadi Julai 1, mwaka huu katika ofisi za TFF Karume, Dar es Salaam.

Wagombea hao wametakiwa kufika na nyaraka halisi za viambatisho vyote walivyoweka kwenye fomu za maombi. Vyeti vya elimu ya Sekondari viwe vya Baraza la Mitihani (NECTA).

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*