Wanyama amtabiria makubwa Mbwana Samatta

Victor Wanyama katika mahojiano na Patrick Nyembera, Azam TV. Kulia ni Mbwana Samatta

Mwanasoka nguli anayekipiga katika klabu ya Tottenham Hotspurs ya England Victor Wanyama amemtabiria makubwa nyota wa Tanzania anayekipiga nchini Ubelgiji, Mbwana Samatta.

Akizungumza katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye kipindi cha Soka Klab, Wanyama amesema kwa jinsi anavyomuona Samatta, anaamini kuwa huyo ndiye mchezaji atakayemfuata kusakata kabumbu katika ligi kuu ya England kutokana na bidii na uwezo alionao.

Amesema katika msimu uliopita Samatta alionesha kiwango cha hali ya juu kilichomkuna hata yeye, na kumshauri aendelee na makali hayo hayo msimu ujao ili asiendelee kucheza Ubelgiji.

Wanyama ambaye pia katika safari yake ya soka amepitia Ubelgiji, amesema yeye na Samatta wanafahamiana, na anatamani kuonana naye huku akikubali pia viwango vya baadhi ya wachezaji wa kitanzania akiwemo golikipa Juma Kaseja

Wanyama na Samatta wote wapo nchini kwa mapumziko na leo Wanyama ametembelea studio za Azam TV na kushangazwa na mambo mengi ikiwemo ubora wa studio pamoja na umahiri katika utayarishaji wa maudhui ikiwemo urushwaji wa moja kwa moja wa ligi kuu ya Tanzania.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*