Habari njema kwa watumishi waliofutwa kazi kisa vyeti feki

Serikali imesema kuwa watumishi wa serikali ambao wamekutwa na vyeti feki na kukata rufaa
wakielezea kuwa vyeti vyao ni halali, itajulikana mwezi huu mwishoni ambapo uamuzi kuhusu
rufaa zao utatolewa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Dk Laurian Ndumbaro alipokuwa akiongea na watumishi wa halmashauri sita za
Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani humo.
Kiongozi huyo alisema mchakato wa kuvihakiki unakaribia kumalizika na karibuni uamuzi kuhusu
wao utatolewa.

“Tunatarajia hadi kufika Juni 30 mwaka huu, wale wote ambao walikata rufaa baada ya kubainika
kuwa na vyeti vya kughushi tutatoa majibu ya rufaa zao, ambazo tulikuwa tukiendelea kuzipitia kwa
makini.
Watumishi hao 9,932 waliokuwa katika orodha aliyokabidhiwa Rais Magufuli walitakiwa
kuondoka katika utumishi wa umma baada ya kubainika kuwa na vyeti vya kughushi.
Wale ambao waliona kuwa wameonewa walipewa nafasi ya kukata rufaa ambapo ndio maamuzi
ya rufaa zao yatatolewa mwishoni mwa mwezi huu.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*