Magoli ya Kichuya yaiweka Stars pazuri

Magoli mawili ya Shiza Kichuya dakika ya 12 na 18 kipindi cha kwanza magoli ambayo yalidumu hadi mechi inamalizika na kuipa Stars ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Malawi.

Ushindi wa Stars unaifanya Stars iongoze Kundi A wakati Malawi wanakamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa kundi hilo lenye timu za Malawi, Mauritius na Angola. Kundi B kuna timu za Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbamwe.

Kichuya amefunga goli la kwanza baada ya kupokea pasi kutoka kwa Simon Msuva, Kichuya alirudi tena kambani kwa mara ya pili akipiga shuti la chinichini lililomshinda golikipa wa The Flames Ernest Kakhobwe.

Baada ya mchezo huo, Kichuya ametangazwa Man of the Match baada ya kuonesha kiwango safi ikiwa ni pamoja na kufunga magoli mawili yaliyoisaidia Stars kupata pointi tatu.

Timu mbili (vinara wa kila kundi) watafuzu hatua ya robo fainali ambako watakuna na timu za Zambia, Botswana, Afrika Kusini, Namibia, Lesotho na Swaziland ambazo zenyewe zimepangwa kuanzia robo fainali zikisubiri washindi wa Kundi A na B kucheza robo fainali.

Tanzania ‘Taifa Stars’: Manula, Gadiel, Banda, Nyoni, Mbonde, Mao, Msuva (Chona 88′), Ramadhani (Ramadhan 80′), Yassin, Kopombe, Maguli (Abed 63′).

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*