Okwi atua Dar es salaam tayari kujiunga na msimbazi

Baada ya mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba SC Zacharia Hans Pope kuthibitisha kuwa mshambuliaji wao wa zamani wa kimataifa wa Uganda Emanuel Okwi anaingia Dar es Salaam Jumamosi ya June 24, usiku wa June 24 ni kweli ameingia Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa kimataifa wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Arnold Okwi akiambatana na Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam leo tayari kusaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na klabu ya Simba kwa mara ya tatu

Kwa taarifa za awali mshambuliaji huyo aliyewahi kuichezea Simba kwa nyakati mbili tofauti, atajiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili kabla ya kurudi kwao Uganda akisubiri maandalizi ya msimu mpya wa Ligi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*