Matumizi mabaya ya ofisi yamuondoa mwenyekiti Halmashauri ya Buhigwe Kigoma

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, limepiga kura ya kumuondoa madarakani Mwenyekiti wao, Elisha Bagwanya, kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi.

Mwenyekiti huyo anakabiliwa na tuhuma saba ikiwemo kufanya kazi ya ukandarasi na halmashauri anayoiongoza kupitia kampuni yake, iitwayo Buyenzi General Supplies, kazi ya mradi wa maji wa Nyamugali ambao ni mbovu.

Tuhuma nyingine ni pamoja na kutumia trekta la halmashauri kulimia shamba binafsi lenye ukubwa wa ekari kumi, lililopo Kijiji cha Bweranga.

Kutokana na tuhuma hizo, wajumbe wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo waliamua kupiga kura na hatimaye kura 20, kati ya 27, zilizopigwa, zilimtaka kiongozi huyo kuachia madaraka.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa Azam TV, Jacob Ruvilo aliyepo Kigoma, Mwenyekiti huyo alikuwepo kushuhudia yaliyokuwa yakiendelea katika mkutano huo

chanzo azam tv

Facebook Comments