Simba yakanusha tetesi za kumsajili Niyonzema na Ngoma

Uongozi wa Klabu ya Simba umekanusha kuwa na mazungumzo au kutaka kumsajili kiungo Haruna Niyonzima aliyeachana na Klabu yake ya Yanga hivi karibuni.

Makamu wa Rais wa Simba, SC Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema hadi sasa uongozi wa klabu hiyo haujapata taarifa yoyote kutoka kwenye kamati yake ya usajili kuhusu Niyonzima, hivyo anashangaa na jinsi ambavyo watu wamekuwa wakimuhusisha nyota huyo wa Rwanda na klabu ya Simba.

Kaburu pia amekanusha tetesi za usajili wa Donald Ngoma kutoka Yanga na kusema kuwa anajua Ngoma ni mchezaji wa Yanga na wao kama Simba hawana mpango naye.

Amesisitiza kuwa mambo yote kuhusu usajili yanayofanyika Simba SC, huanza kwenye kamati ya usajili na kisha huwekwa wazi, hivyo wao kama uongozi bado hawajatoa tamko lolote kuhusu wachezaji hao.

“Mpaka sasa hatujapokea jina la Ngoma wala Niyonzima kutoka kwenye kamati ya usajili, kwahiyo ni vyema mkasubiri tamko rasmi la uongozi kuliko kukaa na uvumi,” amesema Kaburu.

Facebook Comments