Jay Z amuomba msamaha Beyonce

Ilikuwa ni mwanamuziki Beyonce katika wimbo wake uliopewa jina la “sorry” ambao unaeleza kwamba Jay Z yupo na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine ajulikanaye  kwa jina anaitwa Becky.

Lakini hata hivyo mashabiki wa Jay Z nao wanafuatilia kwa umakini albamu iliyoachiwa jana Alhamisi usiku inayodaiwa kama ni majibu ya wimbo wa mwanamama huyo mwenye watoto watatu Beyonce katika wimbo wake wa “sorry”.

Katika mashairi yake kwenye wimbo huo, Jay Z ameimba kuwa “Ningependa kufa kwa si aibu yote,”.

Jay Z mwenye umri wa miaka 47 kwenye wimbo huo anaonekana kutubu kutokana na kukosa uaminifu kwa mkewe Beyonce ambaye hivi karibuni amejifungua watoto mapacha.

Katika kutubu huko, Jay Z anaelezea suala lake la kukosa uaminifu, pamoja na mgongano wake na Solange Knowles mdogo wa mkewe uliotokea miaka miwili iliyopita.

Jay Z amesema kwamba watoto wake ndiyo waliomsukuma kutambua makosa yake, sanjari na kuelezea watoto wake hao mapacha kuwa siyo wa kupandikizwa kama inavyosemekana.

Mashairi ya wimbo wake huo mpya wa 4:44 pia yanaelezea namna anatamani kufa kutokana na aibu ya matendo yake iwapo watoto wake watajua alichokifanya.

Jay Z na Beyonce kwa sasa wana watoto watatu ambapo binti yao wa kwanza ni Blue Ivy mwenye miaka mitanoipokea mapacha, kijana na wa kike.

Facebook Comments