‘Kocha wa Simba’ kutua Gor Mahia

Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka nchini Kenya Gor Mahia wamethibitisha kuwa kocha wao mpya Dylan Kerr atajiunga na timu hiyo Julai 8 kabla ya kusafiri kuja Tanzania kwaajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Everton ya England.

Kerr aliyeifundisha Simba msimu wa 2015/2016 atarejea kwenye ardhi ya Tanzania Julai 13 pindi mabingwa hao wa Super Cup 2017 watakapocheza na Everton katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kocha huyo raia wa Uingereza hakuifundisha Simba kwa mafanikio yoyote, kwani alidumu kwa nusu msimu pekee kabla ya kufungashiwa virago na nafasi yake kuchukuliwa na Golan Kopunovic

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*