NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imepokea kibali Kumb. Na. FA 170/374/01/27 cha tarehe 14 Julai, 2017 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Kibali Kumb. Na. FA.102/282/02B/13 cha tarehe 30 Juni, 2017 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni anawatangazia wananchi wote raia wa Tanzania wenye sifa kuomba nafasi zilizoorodheshwa hapo chini.
MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III- (NAFASI 31)
Sifa za Mwombaji
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
Kazi na majukumu ya Mtendaji wa Mtaa
Katibu wa kamati ya Mtaa
Mtendaji Mkuu wa Mtaa
Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Mtaa
Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa
Msimamizi wa Utekelezaji wa Sheria ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Mtaa
Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama
Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umaskini katika Mtaa
Kusimamia ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote
Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa
Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata
Ngazi ya mshahara ni TGS B sawa na Shilingi 390,000/= kwa mwezi
MTUNZA KUMBUKUMBU MSAIDIZI DARAJA LA II (NAFASI 5)
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au cha Sita (VI) waliohudhuria mafunzo ya Utunzaji wa Kumbukumbu nakupata cheti cha NTA LEVEL 5 katika mojawapo ya fani za Afya,Masjala, Mahakama na Ardhi
Kazi na Majukumu
Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji
Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/ nyaraka
Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu
Kuweka kumbukumbu (barua,nyaraka n.k) katika mafaili
Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali
Ngazi ya mshahara ni TGS B sawa na Shilingi 390,000/= kwa mwezi
KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (NAFASI 1)
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (IV) waliohudhuria mafunzo ya Uhazili nakupata cheti cha NTA LEVEL 5. Wawe wamefaulu somo la hati mkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya kutumia kompyuta kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali nakupata Cheti katika programu za Windows,Microsoft Office,Internet,E-mail na Publisher.
KAZI NA MAJUKUMU YA KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III
Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida
Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa
Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba za kazi nyingine zilizopangwa kutekelezwa katika Ofisi anayofanyia kazi na kumuarifu mkuu wake kwa wakati unaohitajika
Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za hapo Ofisini
Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao
Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika Sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika
Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi
Ngazi ya mshahara ni TGS B sawa na Shilingi 390,000/= kwa mwezi
MSAIDIZI WA HESABU (NAFASI 2)
Kuajiriwa wenye Cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotambuliwa na NBAA, waombaji wawe na uzoefu wa kazi zaidi ya mwaka (1) katika fani hiyo
KAZI NA MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA HESABU.
Kuandika na kutunza “register”zinazohusu shughuli za uhasibu
Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha
Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu
Kupeleka barua/ nyaraka za Uhasibu benki Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.
Ngazi ya mshahara ni TGS B sawa na Shilingi 390,000/= kwa mwezi
NB. Kwa nafasi ya Msaidizi wa Hesabu itakuwa ni kwa Mkataba wa Mwaka mmoja na waombaji wawe tayari kufanya kazi katika Vituo vya Afya.
MASHARTI KWA UJUMLA
Mwombaji awe raia wa Tanzania na awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni
Mwombaji awe na Umri usiozidi miaka 45 na awe hajawahi kupatikana na kosa lolote la jinai, kufungwa jela au kufukuzwa kazi katika Utumishi wa Umma
Waombaji waambatishe maelezo yao binafsi (C.V)
Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya taaluma, vyeti vya kidato cha (IV au VI), cheti cha kuzaliwa na picha mbili za rangi za hivi karibuni na ziandikwe majina nyuma
“Testemonials, provisional results, Statment of Results hati ya matokeo ya kidato cha nne na sita (FORM IV and FORM VI RESULT SLIPS) HAVITAKUBALIWA
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika TCU na NACTE na taarifa ya uhakiki iambatishwe kwenye maombi
Uwasilishwaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria
Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono
Mwisho wa kupokea barua za Maombi ni tarehe 15.08.2017 saa 9:30 alasiri.
Maombi yatumwe kwa Anuani ifuatayo:
Mkurugenzi,
Halmashauri ya Manispaa Kigamboni,
S.L.P 36009,
Kigamboni, Dar es Salaam.
Imetolewa Na :
Stephen E. Katemba
MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA KIGAMBONI

Facebook Comments