Wazee wa Msimbazi wamkataa MO wagomea mkutano.

Mambo ya umiliki wa Klabu ya Simba pamoja na kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo bado yanaendelea kupata kipingamizi ambapo wazee wa klabu hiyo wameliamsha dude kwa mara nyingine.

Baraza la Wazee wa Simba, leo Jumapili wamekutana na waandishi wa habari na kusema msimamo wao ni kuwa hawatambui mikutano iliyotajwa kuwa itafanyika Agosti 13 na 10, mwaka huu kwa kuwa umeagizwa kufanyika na viongozi wanaokaimu nafasi ya uongozi wa juu klabuni hapo huku viongozi wenyewe wakiwa bado mahabusu.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika makao makuu ya Klabu ya Simba, Mzee Hamis Kilomoni alisema hawawezi kukubali na wala hawatambui hiyo mikutano ya wanachama iliyopangwa kufanyika siku hizo mbili.

‚ÄúViongozi wetu wakuu wapo mahabusu, tutafanyaje mkutano wakati tukiwa hatujui hatima ya viongozi wa juu, haiwezekani, pia kuhusu umiliki wa klabu, tulishampa Mo (Mohamed Dewji) nafasi atuletee hoja zake mezani juu ya nia yake ya kutaka kuimiliki Simba lakini hajafanya hilo, hivyo sisi hatutakubali na wala hatuafiki mkakati huo”, alisema mzee Kilomoni.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*