TAMBWE AFURAHIA MSUVA KUONDOKA

Mkali wa mabao kwenye kikosi cha Yanga, Tambwe amesema kuondoka kwa Msuva kutarahisisha yeye kurudisha tuzo yake ya ufungaji bora msimu ujao

Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe amesema kuondoka kwa kiungo Simon Msuva, kumerudisha uhakika wa kurudisha tuzo yake ya mfungaji bora ambayo ameikosa msimu uliopita.

Tambwe amesema, amepania kuipaisha timu yake baada ya kufanya vibaya msimu uliopita kutokana na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

“Vipo vitu vingi vinanifanya nifanye mazoezi kwa bidii ili kufanya vizuri msimu ujao kwanza ni kurudisha shukrani kwa uongozi wa Yanga kwa kuonyesha imani na mimi baada ya kuniongeza mkataba wa miaka miwili lakini kingine ni kutaka kuirudisha Yanga kwenye nafasi ya,”alisema Tambwe.

Amesema kama hatapata majera kama ilivyokuwa msimu uliopita haoni sababu za kumfanya ashindwe kuwa mfungaji bora msimu ujao.

Amesema mtu pekee aliyekuwa na uwezo wa kushindana nae kwa ufungaji katika soka la bongo ni Simon Msuva ambae kuondoka kwake kunamfanya ajihisi ana wajibu wa kuziba pengo lake.
“Msuva alikuwa anafunga mabao zaidi ya 10 karibu kila msimu, hakuna aliyefanya hivyo zaidi yake. Sasa huyu ndie alikuwa mshindani wangu,”amesema Tambwe.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*