Mkemia: Mkojo wa Masogange umebainika kuwa na heroin

Kisutu kuwa sampuli ya mkojo wa msanii Agnes Gerald maarufu kama Deal ama Masogange (28) umebainika kuwa na dawa ya kulevya aina ya heroin.

Akitoa ushahidi leo Jumatano mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, shahidi huyo wa kwanza wa upande wa mashtaka, akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula,
ameiambia mahakama kuwa mnamo February 15, 2017 askari wawili kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, Koplo Sospeter na WP Judith, walimfikisha Masogange ofisini kwake kwa lengo la
kumfanyia vipimo vya mjono wake.

Alisema baada ya kuwapokea, alimsajili Masogange na kumpa namba ya mahabara 446 /2017 na kisha kuwakabidhi kifaa maalum kwa ajili ya kuweka sampuli ya mkojo.
Alidai baada ya kupokea sampuli ya mkojo ya Masogange alifanyia uchunguzi kwa kutumia kemikali na

kubaini kuwa mkojo wake una chembechembe za dawa za kulevya aina ya heroin ambazo kwa
kitaalamu zinajulikana kama Diacety Imophine.

Aidha, alisema uchunguzi zaidi ulibaini chembechembe za dawa nyingine ya kulevya aina ya Oxazepam.
Shahidi huyo alidai baada ya kufanya uchunguzi huo, aliandaa taarifa ya uchunguzi kuhusiana na sampuli hiyo ya mkojo ambapo aliisaini yeye mwenyewe na kuthibitishwa na kaimu mkemia mkuu wa serikali.
Shahidi huyo alimtambua Masogange kwa ndiye aliyepelekwa kuchukuliwa sampuli hiyo ya mkojo ofisini kwake.
Pia alidai anaweza kuitambua taarifa hiyo ya uchunguzi kutokana na kuwepo kwa saini yake, muhuri wa moto wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali. Pia ameomba mahakama kupokea vitu
hivyo kama kielelezo cha ushahidi katika kesi hiyo.

Hata hivyo, mawakili Nehemiah Nkoko na Reuben Simwanza ambao wanamtetea Masogange wamepinga taarifa hiyo ya uchunguzi wakitaka isipokelewe na mahakama kwa madai haijakidhi vigezo vya sheria.

Facebook Comments