Magufuli aiwashia moto Mgambo JKT Tanga

Rais John Magufuli, leo Alhamisi Julai 3, amemwamuru mkuu wa kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya mgambo iliyopo wilayani Handeni mkoani Tanga, kuliachia eneo walilopewa miaka saba iliyopita kwaajili ya kujenga kiwanda.

Hatua hiyo ya rais Magufuli imekuja baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa eneo hilo kulalamikia ukosefu wa ardhi ambayo ingewawezesha kufanya shughuli za uzalishaji, wakati eneo hilo lipo tu na jeshi limeshindwa kutekeleza kile walichopaswa kufanya.

Dkt. Magufuli amemwambia mkuu huyo wa kambi ya JKT mgambo ya tanga ambaye alimwita mbele ili kuelezea kuhusu swala hilo la ardhi, ya kwamba kama wanadhamira ya kujenga kiwanda basi wakajenge kambini kwao ambako kunatajwa kuwa na eneo kubwa na itakuwa rahisi kukihudumia.

Rais Magufuli yupo safarini kuelekea mkoani Tanga kwaajili ya shughuli ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta kutoka Ohima Uganda mpaka bandari ya Tanga, na alisimama eneo la Mkata ili kuwasalimu wakazi wa eneo hilo.

Bomba hilo ambalo jiwe la msingi la ujenzi wake litawekwa Agosti 5, na rais Magufuli na mwenzake rais Yoweri Museveni wa Uganda, linatajwa kuwa na urefu wa zaidi ya kilometa 1,425, huku zaidi ya kilometa 1,100, zitakuwa Tanzania.

Facebook Comments