Niyonzima baada ya Simba Day kaitaja Yanga ni club pekee duniani

Baada ya headlines za muda mrefu kuhusiana na Simba kumsajili kiungo wa kimataifa wa Rwanda aliyekuwa anacheza Yanga Haruna Niyonzima, leo walimtambulisha mbele ya mashabiki na kupata fursa ya kucheza game yake ya kwanza ya Simba Day akiwa Simba.

Haruna ambaye alicheza kuanzia kipindi cha pili baada ya game alijibu maswali ya waandishi wa habari na kuishukuru Yanga kwa muda wote ambao ameichezea lakini ndio timu pekee ambayo amewahi kuichezea kwa muda mrefu zaidi.

“Najua wapenzi wa Haruna wameumia mimi kuhama Yanga lakini mimi nasema yote ni maisha tu, mimi ni mchezaji wa mpira siwezi kujua nitaishia wapi kikubwa ni kufanya kazi yako pia nawashukuru Yanga”>>> Niyonzima

“Unajua Yanga ni timu pekee ambayo nimecheza misimu mingi sana kuliko timu zote duniani nilizowahi kuzichezea hivyo ni jambo la kuwashukuru nimeishi nao vizuri mashabiki, wapenzi wa Haruna na watu wote waliyonionesha ushirikiano nikiwa Yanga” >>> Niyonzima

Facebook Comments