Bill gates atua Tanzania,tembelea kijiji cha Kicheba wilayani Muheza Tanga

Bill Gates akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa wilaya ya Muheza akiwamo Mkuu wa Wilaya Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi, Hajat Mwanasha Tumbo na Mbunge Mhe Adadi Rajabu (wa nne kulia) katika kata ya Kicheba Wilayani humo mkoani Tanga leo

William Henry Gates III maarufu kama Bill Gates na Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft iliyomfanya kuwa mtu tajiri namba moja duniani na mwanzilishi wa mashirika lukuki yasiyo ya kiserikali yenye kusaidia jamii yupo nchini.

Leo ametembelea kijiji cha Kicheba wilayani Muheza katika mkoa wa Tanga kwa lengo la kuangalia maswala mbalimbali ya afya ikiwemo utumiaji wa dawa za mabusha, matende ili kuangalia ni namna gani anaweza kusaidia kwenye sekta hiyo ya Afya.

Bill Gates amesema ataendelea kusaidia kwenye magonjwa 10 kati ya 18 ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kama azimio LA London LA mwaka 2012 yaliyoainishwa na Shirika la afya Duniani(WHO) ambalo linalenga kutokomeza na kudhibiti magonjwa hayo had I ifikapo mwaka 2020 na mwaka 2025.

Kila mwaka tajiri huyo hutoa kiasi cha dola milioni 90 kwa bara LA afrika na Asia katika kutokomeza magonjwa hayo

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi, Hajat Mwanasha
Tumbo (kushoto) akiwa na Bill Gatesbpamoja na mmoja wa viongozi wa
kinamama wa wilaya hiyo katika kata ya Kicheba Wilayani humo mkoani
Tanga leo
Bill Gates akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa wilaya ya Muheza
akiwamo Mkuu wa Wilaya Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi,
Hajat Mwanasha Tumbo na Mbunge Mhe Adadi Rajabu (wa nne kulia) katika kata
ya Kicheba Wilayani humo mkoani Tanga leo
Bill Gates akiwasili na kusalimiana na uongozi wa wilaya ya Muheza katika
kata ya Kicheba Wilayani humo mkoani Tanga leo.
Kujua mengi kuhusu Bill Gates

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*