MAKONDA:YALIYOTOKEA YAMETOKEA TUGANGE YAJAYO

RUGE azua tafrani kuhusu kupatanishwa na Makonda na awalaumu Tef kwa kuwaita bila kuzungumza nao pembeni. TEF, wajitetea wasema waliongea na kukubaliana. Muafaka waonekana kuwa mgumu kwani wahusika bado waonekana kuwa na mvutano katika mkutano huo.

YALIYOTOKEA YAMETOKEA TUGANGE YAJAYO: Makonda na Jukwaa la habari wayamaliza.Asema hataki kufukua makaburi, waandishi wa habari wamtaka aombe msamaha. Mkutano unaendelea katika Hotel ya Holiday Inn.

BALILE: Tumesikiliza pande zote mbili na kugundua kuna sehemu ya mawasiliano katikati ilikatika na hivyo tumeona tuyamalize kwa manufaa ya taifa.Makonda agoma kuomba radhi, kwa madai kuwa hakupewa nafasi ya kusikilizwa.

TEF watangaza kumfungulia rasmi mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Licha ya mkutano wenyewe kumalizika kwa mvutano. Wasema wamuunga mkono rais Magufuli kwa jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo.

Facebook Comments