Polisi Tabora wakamata gunia 70 za bangi

Jeshi la Polisi mkoani Tabora limekamata shehena ya bangi ikiwa na magunia sabini katika msitu wa hifadhi ya Igombe ambapo watu wapatao 15 wanashikiliwa kwa kujihusisha na Kilimo cha bangi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, SACP Wilbroad Mutafungwa amesema katika msako mkali ulioendeshwa na jeshi hilo kwa kushirikiana na maafisa wa Maliasili wamefanikiwa kukamatwa kwa magunia hayo ikiwa ni kiwango kikubwa kukatawa.

Mutafungwa amesema watuhumiwa hao kwa sasa wako chini ya ulinzi na watafikishwa mahakamani punde uchunguzi ukikamilika.

Facebook Comments