Vurugu zalipuka baada ya upinzani kupinga matokeo

Waandamanaji wawili wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi katika mji mkuu wa Nairobi, Kenya leo, Jumatano kufuatia vurugu zilizolipuka baada ya kiongozi wa upinzani kudai kuwa matokeo ya uchaguzi huo yamechezewa huku rais Uhuru Kenyatta akionyesha kushinda.

Mpigapicha wa shirika la habari la AFP ameshuhudia mwathirika ambaye ni kijana mdogo akiwa na jeraha kubwa la risasi kichwani, huku afisa wa juu wa polisi akithibitisha watu wawili kuuawa wakati wa kuzuka kwa ghasia hizo huko katika makazi holela ya Mathare.

“Walikuwa ni sehemu ya kundi la waandamaji katika eneo hilo na polisi walipelekwa kwaajili ya kutuliza ghasia,” alisema afisa huyo wa polisi.

“Tumeambiwa kuwa wengi wao walikuwa ni wezi ambao wamechukua nafasi hiyo na kukiuka amri ya polisi. Wawili wamejeruhiwa vibaya.”

Japheth Koome, Mkuu wa polisi mjini Nairobi, amesema watu hao wawili waliouawa walikuwa “wakijaibu kuwashambua maofisa wetu kwa panga na ndipo maofisa wetu hao walipowalipua kwa risasi.”

Mpigapicha wa AFP ameshuhudia mapanga yakiwa yenye damu yakiwa ardhini katika eneo hilo lenye ghasia.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*