Wateja 200 wakamatwa kwa kutodai risiti za TRA

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha imeendesha msako wa kuwabaini wanunuzi wasiodai risiti pindi wanapofanya manunuzi au kupata huduma pamoja na wafanyabiashara ambao hawatoi risiti na kusema kuwa takribani watu mia mbili wamekamatwa tangu kuanza kwa msako huo.

Meneja msaidizi wa Operesheni hiyo, Alex Katundu, amethibitisha kukamwatwa kwa watu wasiodai risiti pamoja na bidhaa mbalimbali ambazo wanunuzi hao hawakupatiwa risiti.

Baadhi ya wananchi waliokamatwa wamekiri kutodai risiti wakati walipofanya manunuzi na kusema kuwa hawakufanya kusudi na kuwataka wananchi wengine kujifunza utaratibu huu ambao haujazoeleka na watanzania walio wengi

Kwa mujibu wa TRA opereshini hiyo ni endelevu ili kuwafanya watanzania kuwa na utamaduni ambao unasaidia katika ukusanyaji wa mapato kwa serikali.

“Muuzaji akishindwa kutoa risiti faini yake ni kuanzia milioni 3, hadi 4, huku mnunuzi ambaye hatodai risiti faini yake ikianzia shilingi elfu thelathini.”

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*