NAFASI 200 ZA KAZI-TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA

Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapo chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Ofisi za Mahakama ya Tanzania zilizoko katika Mikoa mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi. Nafasi hizo ni Hakimu Mkazi Daraja la II – (TJS 2) nafasi 100, Katibu Mahsusi Daraja la III – (TGS B) nafasi 20, Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – (TGS B) nafasi 45, Mpokezi – (TGS A) nafasi 1, Dereva Daraja la II – (TGOS A) nafasi 10, Mlinzi (TGOS A) nafasi 21 na Afisa TEHAMA Daraja la II Nafasi 3 (TGS.E).

Mwisho wa kupokea barua za maombi hayo ni tarehe 04/09/2017 saa 9:30 Alasiri.

2.0 Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji zikionyesha anwani sahihi
pamoja na namba ya simu na kuambatisha:-

– Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.

– Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV).

– Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.

– Picha mbili za rangi (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni.

NB. Nakala za vyeti vya taaluma na vya kidato cha nne/sita vithibitishwe na Hakimu/Wakili

anayetambuliwa na Serikali (True copies of the originals).

3.0 Aidha, inasisitizwa kwamba:-

3.1 Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 44

3.2 Waombaji wakazi toka maeneo husika na wenye sifa zilizoainishwa katika tangazo hili, watafikiriwa kwanza na kupangiwa kazi katika maeneo husika.

3.3 Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa wilaya anayoishi mwombaji.

3.4 Waombaji walio katika Utumishi wa Umma wapitishe maombi yao kwa waajiri wao wa sasa.

3.5 Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa Umma waeleze kwamba waliacha kazi Serikalini na sababu ya kufanya hivyo.

3.6 Waombaji watakao shinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania.

3.7 Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na TCU/NACTE.

3.8 Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa kirefu.

3.9 Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba nyuma ya bahasha

watakazotumia maombi yao.

3.10 Waombaji wasiwe walioachishwa/kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa Umma.
3.11 Mwombaji asiandike barua zaidi ya moja kwa ajili ya kuomba nafasi moja.

3.12 Waombaji wote wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia mojawapo ya masharti yaliyotajwa hapo juu, maombi yao hayatashughulikiwa.

4.0 Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi

wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P. 8391 , DAR ES SALAAM.

Imetolewa na ;-

Katibu,

Tume ya Utumishi wa Mahakama,

S.L.P 8391,
DAR ES SALAAM.

BOFYA HAPA KUTEMBELEA TOVUTI YA MAHAKAMA KWA MAELEKEZO MUHIMU

Facebook Comments