Rugemalira, Harbinder Sethi ngoma bado nzito Kisutu

Kesi inayomkabili mkurugenzi wa kampuni ya VIP, James Rugemalira na mwenzake Harbinder Singh Sethi ambaye ni mmiliki mwenza wa zamani wa kampuni ya IPTL, iliyopangwa kusikilizwa jana kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepigwa kalenda hadi Agosti 31.

Awali watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza mnamo Juni 19, mwaka huu, na kusomewa makosa sita ikiwemo upotevu wa fedha zaidi ya bilioni 300, kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Baadaye makosa hayo yaliongezeka na kufikia 12, yote yakiwa ya uhujumu uchumi huku yote hayo yakiwa hayana dhamana kisheria.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*