Penzi la Wema na Idris kuzaliwa upya?

Penzi lililokufa kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita kati ya msanii wa komed Tanzania Idris Sultan pamoja na mrembo wa Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu, huenda likazaliwa upya baada ya wawili hao kuanza mazungumzo kiaina kupitia mitandao ya kijamii.

Mazungumzo hayo yameibuka ikiwa ni siku moja imebaki kuelekea siku ya uzinduzi wa ‘brand’ mpya ya kibiashara ya Idriss ijulikanayo kama Sultan X Foremen, inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho Agosti 20, 2017.

Kuelekea siku hiyo, Wema Sepetu kupitia mtandao wa Instagram, ameibuka na kumpongeza Idris kwa hatua hiyo, huku akiweka wazi kuwa hawezi kuficha hisia zake na kumwagia misifa kwamba ubora ndicho kitu pekee kinachomtambulisha mpenzi wake huyo wa zamani.

“Nikisema sitojivunia ntakuwa ni muongo na mnafiki… Proud of you sana… Cant wait for these babies to launch… I’m sure zitakuwa Killer… Cause one thing I know is that “Classy” defines you alot better than anything…#SultanXForemen … Goodmorning World…” Ameandika Wema Sepetu huku akitupia picha ya Idris.

Saa chache baada ya ujumbe huo, Idris naye akatoa neno akionesha kushangazwa na mtu ambaye hakuwa na mawasiliano naye kwa muda mrefu kuibuka na kuanza kumpongeza, lakini akawataka watu wasishtuke kwa kuwa Wema ni mke wake na mke huwa haachwi hata aolewe na mwanaume mwingine.

“MOOD: Unakuta kakuposti tu wakati mmekulana block hadi kwenye email … Dahhh we mwanamke utakuja uniue .. Thank you mke … Msishtuke, kuanzia lini mke anaachwa hata aolewe.” Ameandika idris

Kwa hatua hiyo ni wazi kuwa huenda uzinduzi huo ukarejesha upya mahusiano kati ya mastaa hawa wawili. Tusubiri tuone.

Hadi sasa haijawa wazi kuwa brand hiyo itakuwa inahusu bidhaa gani, ingawa taarifa zisizo rasmi zinaonesha kuwa huenda ikawa ni viatu

Facebook Comments