TFF YAMUENGUA CHIRWA NGAO YA JAMII DHIDI YASIMBA

Shirikisho la soka Tanzania TFF, limemuengua Obrey Chirwa, kwenye kikosi cha Yanga kitakacho ikabili Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii

Yanga itamkosa mshambuliaji wake wa pembeni katika pambano la Ngao ya Jamii Jumatano Mzambia Obrey Chirwa kutokana na adhabu ya kadi ya kumwangusha refa katika mchezo wa ligi ya Vodacom dhidi ya Mbao FC msimu uliopita.

Msemaji wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Alfred Lucas amesema adhabu ya Chirwa inatumika pande zote mbili kwenye mechi ya ligi pamoja na michuano ya FA.

“Tunawatahadharisha Yanga wasije kumtumia Chirwa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Jumotano dhidi ya Simba kwasababu anatumikia adhabu aliyopata kwenye mchezo wa mwisho wa ligi ya Vodacom msimu uliopita,”amesema Lucas.

Lucas amesema Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji bado haijaketi na kutoa maamuzi hivyo mchezaji huyo ataendelea kuwa nje hadi hapo hukumu yake itakapotoka.

Amesema kama kufikia Jumamosi Kamati hiyo itakuwa haijakutana na kutoa maamuzi Chirwa ataendelea kukaa nje na hiyo inatokana na kanuni na sheria zinazowaongoza.

Hata hivyo Yanga walishamwengua Chirwa kwa wachezaji ambao wataikabili Simba Jumatano kutokana na majeruhi ambayo yanamkabili kwa wiki mbili sasa.

Katika tukio hilo Chirwa na Msuva, walituhumiwa kumwangusha chini kwa makusidi mwamuzi aliyechezesha pambano lao dhidi ya Mbao na kutakiwa kukaanje wakati jambo lao likishuhulikiwa lakini Msuva amehama Yanga na sasa anaichezea Difaal El Jadida ya Moroco

Facebook Comments