Mavunde awapa somo vijana wanaosubiri ajira

Naibu waziri Ofisi ya waziri mkuu, Sera, Bunge, Kazi na Ajira, Anthony Mavunde, amewataka vijana kuchangamkia fursa na kuacha kuisubiri serikali itoe matangazo, iwatafute, iwakusanye na kisha iwape ujuzi.

Mavunde ametoa somo hilo leo Alhamisi Agosti 24 mkoani Mtwara, alipokuwa akizindua mafunzo ya utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi kwa vijana 847.

Vijana walioshiriki kwenye mafunzo hayo ni kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi, Morogoro, Pwani na Dar es salaam.

“Msingi wa maisha ya kijana unaanzia hapa, kijana wa kitanzania jiamini, timiza wajibu wako,” alisema Mavunde.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi wa Azam TV, Mohamed Mwaya, aliyopo mkoani Mtwara, Mavunde amewaomba vijana waliopata fursa ya kuingia kwenye mafunzo hayo, kutumia vizuri fursa hiyo kwa kuwa waaminifu na kuwajibika kama msingi wa mafanikio.

Mavunde pia amewakumbusha vijana hao kujiepusha na vitendo vya tamaa na kuwataka kufuata hatua ili kuyafikia mafanikio.

“Ni kaburi peke yake watu waanza kuchimba kuanzia juu kwenda Chini, lakini maisha yananzia chini kwenda juu,” amesisitiza Mavunde.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*