Msuva atua kuimaliza Botswana

Kiungo Taifa Stars, Saimon Msuva tayari amejiunga na timu hiyo akitokea klabu ya Difaa El Jadidah ya Morocco baada ya shirikisho la soka Morocco na timu yake kumfanyia mpango wa viza ya muda mrefu iliyomwezesha kusafiri.

Ujio wa Msuva unaondoa hofu iliyokuwepo hasa baada ya taarifa za kukwama kwake kutokana na matatizo ya viza yaliyokuwa yakimkabili.

Mchezaji ambaye imeshindikana kuja ni Orgenes Mollel wa FC Famalicao ya Ureno ambako anacheza soka la kulipwa.

Msuva anaungana na nyota wengine waliokwisha kuripoti ni pamoja na Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Elias Maguli (Dhofar FC/Oman), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya) wakati Farid Mussa wa CD Tenerif ya Hispania anatarajiwa kutua leo.

Wengine ambao wako kambini ni makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young Africans).

Pia wamo Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).

Viungo ni Himid Mao – Nahodha Msaidizi (Azam FC), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Shiza Kichuya (Simba SC), wakati Washambuliaji ni Raphael Daud (Young Africans), Kelvin Sabato (Azam FC) na Emmanuel Martin (Young Africans).

Taifa Stars inajiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana utakaopigwa Jumamosi hii katika dimba la Uhuru jijini Dar es salaam.

Facebook Comments