Rais Magufuli ateta na viongozi wa ulinzi na usalama

Rais John Magufuli amekutana kwa mazungumzo na viongozi wakuu wastaafu na wa sasa wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Viongozi hao ni wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza na wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa amesema Rais Magufuli amekutana na viongozi hao leo Agosti 31 kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujenga ushirikiano imara zaidi kati ya wastaafu na waliopo kazini katika kutekeleza majukumu ya ulinzi na usalama wa nchi.

Viongozi hao wamemshukuru Rais kwa kuwaita na kufanya nao mazungumzo, ambayo wamesema yamewawezesha kubadilishana mawazo na kuimarisha ushirikiano kati yao.

Pia, wamempongeza Rais kwa uendeshaji mzuri wa Serikali na hasa katika kusimamia uchumi, kupiga vita rushwa na kujenga nidhamu kwa watumishi wa umma.

Facebook Comments