Yanga yaondoka kwenda kuwakabili Njombe Mji

Kikosi cha Timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, kimeondoka leo kikielekea Njombe tayari kwa mchezo wake dhidi ya Timu ya Njombe Mji, utakachezwa keshokutwa Jumapili katika uwanja wa Majimaji.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, watawavaa timu hiyo mpya katika Ligi ya Vodacom msimu huu wakiwa na kumbukumbu ya sare ya bao 1-1 katika mchezo wao wa kufungua pazia wa ligi hiyo uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten amesema, kikosi hicho kimeondoka jijini kikiwa na wachezaji 26, isipokuwa Amis Tambwe, Beno Kakolanya na Baruhani Akilimali ambao bado wanaendelea na matibabu kufuatia majeraha waliyoyapa.

Amesema, wanataraji mchezo huo utakuwa mgumu kwa madai ya kuwa ugenini, lakini wanaimani wataibuka na ushindi wa pointi tatu.

Naye daktari wa timu hiyo, Edward Bavu, amewataja wachezaji Obrey Chirwa na Geofrey Mwashiuya, wanaendelea na mazoezi mepesi huku wakitarajiwa kuwa katika safari hiyo ya kuelekea Njombe.

Facebook Comments