Simba si wa mchezo Waujaza uwanja wa Azam Complex

Muda mchache  kabla ya Azam kuikaribisha Simba kwenye mechi ya raundi ya pili ya Ligi Kuu, mashabiki wa Simba wameuteka Uwanja wa Azam Complex.

Mashabiki hao wa Simba wamejaza zaidi ya 3/4 ya majukwaa ya uwanja huo ambao hadi ilipofika saa 8.00 mchana, viti vichache ndivyo vilikuwa wazi.

Shabiki wa Simba aliyejitambulisha kwa jina la Kanali kutoka tawi la Ubungo Terminal alisema kuwahi kwao kumetokana na sababu mbili.

“Kwanza vyombo vya usalama vilituomba tuwahi mapema kuingia uwanjani kutokana na uwanja kuingiza watu wachache lakini, pia tuna imani na ubora wa timu yetu kwamba leo tuna nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi

Facebook Comments