Erasto Nyoni hana makuu mtaani kwake

Beki mpya kiraka wa Simba SC, Erasto Nyoni, amaejipambanua kama mtu asiyependa makuu na kuendelea kuishi maisha ya kawaida sana kama ilivyokuwa kabla ya kuwa staa kwenye ulingo wa soka.

Nyoni ambaye pia ni mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), ameonekana akila mihogo ya kukaanga tena iliyowekwa kwenye mfuko wa plastiki (mfuko laini) aliyonunua kutoka kwa muuza bidhaa hiyo mtaani kwake eneo la Tabata Segerea, jijini Dar es Salaam.

Tabia hiyo ya kuvutia ya beki huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi awapo dimbani, imethibitika kwenye kipindi cha Soka Kijiweni, kinachoruka kila siku ya Jumatatu saa moja kamili jioni, kupitia chaneli ya michezo ya Azam Sports2.

Katika kipindi hicho, alishuhudiwa mama mmoja wa eneo hilo analoishi, akimletea vipande hivyo vya mihogo, huku akiwa ameshika pilipili ya maji ambayo pia ilikuwa imewekwa kwenye mfuko laini na kikombe cha maji mkononi.

Mwendesha kipindi hicho Jamal Abbas, alimuuliza mama huyo kama anamfahamu mwanasoka huyo, haraka sana mchuuzi huyo alijibu kwa kutaja jina kamili la beki huyo.

Facebook Comments