Mayweather: Nina wapenzi saba

Bondia Floyd Mayweather amefunguka kuhusu uhusiano wake na kuweka wazi kuwa kwa sasa anamiliki wapenzi saba na kwamba hawezi kuishi na mpenzi mmoja.

Mayweather amedai kwamba endapo atakuwa na mpenzi mmoja atajiona ni kama hana mpenzi na kujihisi mpweke.

Bingwa huyo wa dunia katika ngumi za uzito wa juu, ametaja idadi hiyo ya wapenzi baada ya kuulizwa endapo na mpenzi, ambapo alijibu kuwa yeye si aina ya mwanaume ambaye anaweza kuwa na uaminifu kwa mwanamke mmoja.

“Unaniuliza nina wapenzi wangapi? Ninao kama saba hivi , tena saba wenye bahati,” amejibu Mayweather.

Amefunguka hayo katika mahojiano maalum kupitia channel ya youtube ya Awkward Puppets na kuzungumzia kwa kirefu kuhusu maisha yake binafsi, huku akiweka wazi kuwa hadi sasa anamiliki magari 25 yakiwemo mawili yanayofahamika aina ya Bugatti na Ferrari.

Kuhusu yeye kuendelea na mchezo wa ngumi, bondia huyo amesisitiza kuwa pesa alizopata baada ya kumpiga McGregor hivi karibuni, ndizo za mwisho kutoka kwenye mchezo huo, akimaanisha kuwa hana mpango tena wa kupigana.

“Pambano la mwisho nililopigana lilikuwa ni pambano la pesa, kwa pambano jingine, inabidi wanipeleke nikapigane katika sayari nyingine,” amesisitiza.

Facebook Comments