Polisi Mtwara wadaka watano kuhusika na shambulio

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linawashikilia watu Watano ambao wanadaiwa kuhusika na tukio la kumshambulia kwa silaha hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Masasi, Khalfan Ulaya na kumsababishia kifo kilichotokea Septemba 8 mwaka huu.

Akizungumaza na waandishi wa habari ofisini kwake, kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Naibu Kamishna wa Polisi Lucas Mkondya amesema hatua hiyo imekuja baada ya kufanyika msako mkali ulioanza baada ya tukio hilo, huku watuhumiwa wote wakikiri kuhusika baada ya kuhojiwa.

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limesema kumeibuka tabia ya wizi wa mafuta katika viwanda vya saruji vya Dangote Industries Limited na Mtwara Cement, pamoja na wizi wa vifaa vya ujenzi katika kampuni zinazojenga barabara mkoani humo.

Facebook Comments