PSG, Chelsea zaanza kwa dozi nene UEFA

Jeuri ya pesa imeanza kulipa kunako klabu ya PSG ya nchini Ufaransa ambayo imeanza michuano ya mabingwa barani Ulaya kwa kuishushia dozi ya bao 5-0 timu ya Celtic ya Scotland.

Matajiri hao waliotumia pesa nyingi zaidi kwa usajili msimu huu wametumia mtambo wake mpya wa kuzalisha mabao unaoundwa na Neymar, Mbappe na Cavan kupata mabao hayo ya ugenini.

Kwa upande wa Chelsea waliokuwa darajani, Stamford Bridge wameipa kichapo cha bao 6-0 timu ya Qarabag FK kupitia kwa Pedro, Zappacosta, Azpilicueta , Bakayoko na Batshuayi akifunga mabao mawili.

Matokeo ya mechi zote za ligi hiyo zilizopigwa Jana usiku ni kama ifuatavyo

KUNDI A:
Benfica 1-2 CSKA Moscow
Man United FC 3-0 Basel (Fellaini 35, Lukaku 53, Rashford 84)

KUNDI B:
Bayern Munich 3-0 Anderlecht
Celtic 0-5 PSG (Neymar 19, Mbappe 34, Cavan 40, 85, Lusting 83)

KUNDI C:
Chelsea 6-0 Qarabag FK
AS Roma 0-0 Atletico Madrid .

KUNDI D:
Barcelona 3-0 Juventus (Messi 45, 69 Rakitic 56)
Olympiacos 2-3 Sporting CP

Facebook Comments