Real Madrid kuanza kutetea kombe lake lao

Mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya timu ya Real Madrid leo inaanza kampeni ya kutetea kombe hilo katika mchezo wake wa kwanza hatua ya makundi.

Vijana hao wa kocha Zinedine Zidane ambao wameanza ligi ya Hispania kwa kusuasua kutokana na kulazimishwa sare mbili, leo watakabiliana na APOEL Nicosia katika dimba la Santiago Bernabeu jijini Madrid, Hispania

Real Madrid iko kundi H ambalo linatajwa kuwa kundi gumu zaidi ikiwa pamoja na Dortmund, Tottenham na APOEL Nicosia.

Baada ya kumkosa kwa muda mrefu, leo Real inatarajia kuwa na nyota wake Cristiano Ronaldo ambaye anatumikia kifungo cha mechi tano za ligi kwa kosa la kumsukuma mwamuzi katika mchezo wa kwanza wa ‘Spanish Super Cup’ dhidi ya Barcelona.

Vigogo wengine watakaokuwa dimbani leo ni pamoja na Liverpool ambayo imerejea baada ya kukosekana kwa muda mrefu katika michuano hiyo, Man City, Dortimund, Tottenham na FC Porto.

Ratiba kamili iko hivi:

KUNDI E:
Liverpool Vs Sevilla
Marbor Vs Spartak Moscow

KUNDI F:
Feyenoord Vs Man City
Shakhtar Donetsk Vs SSC Napoli

KUNDI G:
FC Porto Vs Besiktas
RB Leipzig Vs Monaco

KUNDI H:
Real Madrid Vs APOEL Nicosia
Tottenham Vs Dortmund

Facebook Comments