Producer wa muziki THT atoweka siku 5 sasa

Habari za kusikitisha ambazo zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii tangu jana ni kuwa, Mtayarishaji wa Muziki kutoka katika Studio za Tanzania House of Talents (THT), Ema The Boy hajulikani alipo kwa zaidi ya siku 5 sasa.

Taarifa hizo zilizosambazwa na watu mbalimbali zimedai kuwa, hakuna anyefahamu alipo Ema na wala namba zake za simu ya mkononi hazipatikani.

“…hakuna taarifa yoyote kuhusiana na yeye na wala namba zake hazipatikani…,” aliandika nicole_franklyn katika ukurasa wake wa Instagram.

Aidha, imeelezwa kuwa yeyote atakayekuwa na taarifa zozote kuhusu mtayarishaji huyo wa muziki, atoe taarifa kupitia namba, 0656388919, kituo chochote cha polisi au katika Ofisi za Clouds Media Group.

Facebook Comments