Uchaguzi Kenya Kusogezwa Mbele

ume huru ya uchaguzi nchini Kenya leo, Jumatatu imekutana kwaajili ya kuangalia ombi la uwezekano wa kupelekwa mbele ya Oktoba 17, uchaguzi huo.

Ombi hilo limekuja kutoka kwa kampuni ya Safran Morpho ya nchini Ufaransa. Wiki iliyopita kampuni hiyo iliwaomba wakala hao wa kusimamia uchaguzi kuongeza muda hadi Oktoba 26 ili kuruhusu maboresho ya mfumo wa utambuzi wa kura na usafirishaji wa matokeo.

Kampuni hiyo inataka kurekebisha na kuboresha mfumo huo na kuondoa taarifa zozote zilizopo kwaajili ya maandalizi ya marudio ya uchaguzi wa urais uliobatilishwa na Mahakama ya Juu ya nchi hiyo kwa madai haukufuata taratibu, Agosti 8.

Facebook Comments