Yanga yapata faraja kuachiwa kwa Manji leo

KUFUATIA Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kumuachia huru Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, Yussuf Mehboob Manji katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya iliyokuwa inamkabili, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba hatua hiyo ni faraja kubwa kwa wana Yanga.

Mkwasa ameyasema hayo leo Mahakama ya hakimu Mkazi, Kisutu mjini Dar es Salaam baada ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kumuachia huru Manji akisema kwamba upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka hayo dhidi ya mtuhumiwa.

Mkwasa amesema, awali walikuwa na hali ngumu kufuatia mwenendo wa kasi hiyo ulivyokuwa lakini sasa wamefarijika na wanaamini watashikamana kwaajili ya kuijenga timu yao.

Facebook Comments