Diamond na Zari wapiga marufuku kuwajadili mitandaoni

WIKI hii Diamond Platnumz ameachia povu zito kuwaendea watu ambao wamekuwa wakifuatilia uhusiano wake na wanawake ambao amewahi kuwa nao.

Akitumia ukurasa wake wa Instagram, Diamond alisema watu wamuache kwa kuwa amejikita zaidi kuipeleka Bongo Fleva mbele na siyo kuanza kudili na mambo yanayoendelea Bongo.

“Mara Diamond Kamla Huyu, mara sjui naskia anatembea na huyu, Mara Ooh sjui inasemakana juzi alikuwa na huyu…Yaani kila ukiamka limezuka jipya, utazani yangu ina sukari au nakojoa dhahabu…..Hebu niacheni kidogo, niko busy nahangaika kuipeleka Bongo Fleva yetu duniani…. Sijamkaza yoyote na sina mahusiano na yoyote anayetajwa na siku pia nikimaliza mahusiano yangu na aliye South na nikawa na mwingine na ikifikia kuliweka wazi nitaliweka wazi mwenyewe. Maana hakuna kitachonizuia… ndio kwanza nina miaka 28. Sijaoa na hata nikioa naruhusiwa niwe na wake wanne…,” aliandika.

Nae Zari kuoneshwa kukerwa na drama zinazoendelea kupitia kurasa yake ya snapchat aliponda watu wanaoongea kuhusu maisha yake binafsi kuwa wamuache.

“Ati nini? Yule wa wapi? Hana gina ati Mama T. unachako huku. Can I be left out of this drama please! Naomba,” aliandika

Lakini katika moja ya mahojiano Zari amefunguka kuwa wao wapo pamoja ila kwa sasa wanajaribu kuamisha mapenzi yao kuwa siri zaidi.

“Kama heri yake ya kuzaliwa nilimtakia kupitia namba yake ya simu lakini haya mambo yanayoendelea ni drama tu kwa sasa hatutaki mahusiano yetu yawe ya uwazi zaidi bali tunataka kuyapeleka kwa usiri lakini tupo sawa bado,” alifunguka Zari.

Facebook Comments