Diamond Platnumz ashinda tuzo Marekani

Mwanamuziki Diamond Platnumz amezidi kudhihirisha ubora wake katika kuendelea kuinua muziki wa Tanzania (Bongo Fleva) baada ya jana usiku kushinda tuzo nyingine.

Usiku wa Oktoba 8 kutoka Dallas nchini Marekani zilipokuwa zikitolewa tuzo za Africa Muzik Magazine Awards (AFRIMMA), Diamond Platnumz alishinda tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kiume kutoka Afrika Mashariki, kipengele ambacho kilikuwa na jumla ya wasanii kumi.

Facebook Comments