Mwamuzi aondolewa ligi kuu

Kamati ya bodi ya ligi ya uendeshaji na usimamizi wa ligi imemuondoa mwamuzi msaidizi, Grace Wamara kuchezesha ligi kuu ya Tanzania Bara kwa kukosa umakini na kutomsaidia mwamuzi, hivyo kusababisha akubali bao lenye utata la Stand United dhidi ya Mbeya City.

Wamara alikuwa mwamuzi msaidizi namba mbili kwenye mechi hiyo iliyofanyika Septemba 24, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na wenyeji Stand United kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Taarifa ya TFF imeeleza kuwa uamuzi wa kumuondoa Wamara ambaye amerejeshwa katika kamati ya waamuzi ya TFF kwa ajili ya hatua nyingine umefanywa kwa kuzingatia kanuni ya 38(5) ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa waamuzi.

Facebook Comments