Simba, Singida United zalimwa faini

Klabu ya Simba imepigwa faini ya shilingi 500,000 kutokana na timu yake kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi katika mechi dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Septemba 21, mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Adhabu hiyo imetolewa na kamati ya bodi ya ligi ya uendeshaji na usimamizi wa ligi ambayo pia imempa onyo kali kamishna wa mechi hiyo, Maliki Tibabimale kwa kutoripoti kitendo hicho cha Simba.

Katika hatua nyingine Singida United imepigwa faini ya shilingi 500,000 kutokana na mashabiki wa timu hiyo kuingia uwanjani kushangilia ushindi baada ya mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyofanyika Septemba 23, mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Adhabu dhidi ya Singida United imetolewa na kamati hiyo kwa kuzingatia kanuni ya 42(1) ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa klabu.

Facebook Comments