Marufuku kutoa stika bila ukaguzi wa gari -Masauni

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Eng. Hamad Massauni

Serikali imesema inao mpango madhubuti kuhakikisha hakuna stika ya gari yoyote nchini itakayotolewa bila gari kukaguliwa, huku akisema hakuna askari atakayesalia akibainika kutoa stika hizo bure bila gari kukaguliwa.

Kauli hiyo ameitoa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipozungumzia kuhusu kuanza kwa wiki ya usalama barabarani na kuweka bayana wamejipanga kuhakikisha wanamaliza tatizo la ajali za barabarani nchini licha ya kuwepo kwa upungufu katika sheria ya usalama barabarani.

Naibu waziri Masauni amesema kumekuwepo na baadhi ya askari wanaotoa stika za magari holela na kuweka bayana serikali haina masihara wala msalie mtume kwa atakayebainika kufanya hivyo.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*