Mrisho Gambo amtoa wasiwasi Lema

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amemtoa wasi wasi mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema, juu ya hofu ambayo amehisi anayo, kwamba anatengeneza mazingira ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkoani Arusha, Mrisho Gambo amesema hofu anayopata Lema juu yake hapaswi kuwa nayo, kwani hana mpango wa kugombea nafasi hiyo, isipokuwa yeye anatekeleza majukumu yake kama mkuu wa mkoa kwa wananchi wake, huku akimtaka Godbless Lema kutekeleza majukumu yake kwa wananchi, na sio kuleta porojo ambazo wananchi hawazihitaji kwa sasa.

“Godbles Lema, akipita kwenye ziara zake nyingi badala ya kuzungumza maendeleo ya watu wetu, anazungumza kwamba mkuu wa mkoa msione anafanya hivi, kwa sababu anataka ubunge, mi nikisikia hivyo najua ana hofu, amejipima pima akaona pengine kivuli changu kinamtisha, mwambieni aache uoga, mi ni mkuu wa mkoa ambaye halmashauri zote, wabunge wote wapo chini yangu, sijawahi kuwa na wazo tofauti na kazi hii ninayofanya sasa, mwambie tu ahangaike na shida za watu asinihofie mimi”, amesema Mrisho Gambo.

Mrisho Gambo ameendelea kwa kushauri watu wa namna hoyo waache ujanja ujanja, kwani wananchi sasa hivi hawataki usanii.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*